Jumapili 10 Agosti 2025 - 11:15
Mipango ya uvamizi na uharibifu inayofanywa na utawala wa Kizayuni itashindwa na kusukumwa nyuma.

Hawza/ Mkurugenzi wa Hawza Irani alisema: Tuna imani ya hakika kwamba mipango ya uvamizi na uharibifu inayofanywa na utawala huu, kwa baraka ya uelewa wa umma wa Kiislamu, hatua za serikali huru na pia juhudi za wanaharakati huru kote duniani, itashindwa na kusukumwa nyuma.

Kwa mujibu wa  Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah A’rafi, Mkurugenzi wa Hawza Iran, katika mkutano wa mtandaoni wa kimataifa kuhusu Ghaza na Wanazuoni wa Umma uliokuwa na anuani isemayo “Kulaani uhalifu wa kivita unao sababisha ukame wa njaa, kuwalazimisha watu wa Ghaza kuondoka kwa lazima”, uliofanyika kwa lugha ya Kiarabu na kuhudhuriwa na watu mashuhuri wa kielimu na kisiasa kutoka nchi mbalimbali za Kiislamu, alitoa hotuba ambayo maandiko yake ni kama ifuatavyo:

بسم‌الله الرحمن الرحیم

الحمد لله ربّ العالمین بارئ الخلائق أجمعین، ثمّ الصلاة و السّلام علی سیّدنا و نبیّنا و حبیبنا أبی‌القاسم المصطفی محمّد و علی آله الأطیبین الأطهرین و صحبه المنتجبین

Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema katika Qur’ani Tukufu:


وما لکمْ لا تقاتلون فی سبیل الله والْمسْتضْعفین من الرجال والنساء والْولْدان

Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto..
(An-Nisaa, 75)

صدق‌الله العلیّ العظیم

Waheshimiwa wakuu, wanazuoni na wasomi watukufu,

Viongozi na watu mashuhuri katika ulimwengu wa Kiislamu,

Leo tunashuhudia moja ya matukio ya kikatili zaidi na jinai mbaya zaidi dhidi ya ubinadamu katika historia, ambapo utawala wa Kizayuni wenye kupora, ukiungwa mkono moja kwa moja na nguvu za kimfumo zenye jeuri duniani na hasa Marekani yenye jinai, hauendelei tu na uvamizi wa ardhi ya Wapalestina wanyonge — ambayo ni sehemu isiyotenganika na umma wa Kiislamu — bali pia unasisitiza kuendelea na vikwazo vyake vya kishenzi katika Ukanda wa Ghaza wa kuwahukumu wananchi wake jasiri kwa njaa, kuhama kwa kulazimishwa na kifo cha taratibu.

Jinai hizi ni dhahiri kuwa uvunjaji wa wazi wa haki za binadamu na kanuni zote za kimungu, thamani za kidini na maadili ya kibinadamu.

Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Qur’ani Tukufu, miongoni mwa aya tukufu iliyosomwa, ametufaradhishia kuwasaidia wanyonge, na leo watu wa Ghaza wanyonge ndio mfano halisi wa “mustadh’afina” ambao haki zao za msingi kabisa zimeporwa na Wazayuni waporaji, na kuwanusuru ni jukumu la kisheria na kimungu lililoko mabegani mwa kila Muislamu, Na kama alivyosema Mtume Mtukufu Muhammad (saw):

من سمع رجلاً ینادی یا للمسلمین فلم یجبه فلیس بمسلم

Mwenye kumsikia mtu ananadi enyi waislamu na asimjibu, basi si muislamu

Mikataba na makubaliano ya kimataifa yameweka mkazo juu ya ulazima wa kuitikia wito wa wanyonge na kupambana vikali na wavamizi, na kwa uwazi na upana yamepiga marufuku jinai kama mauaji ya kimbari, kuwanyima chakula, kuwahamisha kwa lazima na kuwaua raia wasiokuwa na silaha.

Kwa mujibu wa Kifungu cha Saba cha Mkataba wa Roma, Kifungu cha Pili cha Mkataba wa Kuzuia na Kutoa Adhabu kwa Jinai ya Mauaji ya Kimbari, na Kifungu cha 54 cha Itifaki ya Kwanza ya ziada katika Mikataba ya Geneva, pamoja na katiba na sheria nyingi nyingine za kimataifa, vitendo vya kishenzi vya utawala wa Kizayuni ni mfano halisi wa uhalifu wa kivita, mauaji ya kimbari na jinai dhidi ya ubinadamu.

Wazayuni wavamizi, kwa kuendelea na vizuizi vyao vya kikatili, kishenzi na aibu katika Ukanda wa Ghaza, na kuwanyima watoto, wanawake na wazee maji na chakula, na kulenga hospitali na shule kwa mabomu ya kikatili, ni mfano halisi wa waharibifu ambao Mwenyezi Mungu amewataja katika Qur’ani Tukufu:


إنّما جزاء الّذین یحاربون اللّه ورسوله ویسْعوْن فی الْأرْض فسادًا

Basi malipo ya wale wanao mpiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakawania kufanya uchafuzi katika nchi..
(Al-Maida: 33)

Na pia amesema kuhusu wao:

وإذا تولّیٰ سعیٰ فی الْأرْض لیهْلک الْحرْث والنّسْل ۗ واللّه لا یحبّ الْفساد

Na anapo tawala hufanya juhudi katika nchi kwa kufisidi humo na kuteketeza mimea na viumbe. Na Mwenyezi Mungu hapendi ufisadi.
(Al-Baqara: 205).

Na kwa upande mwingine, Amirul-Mu’minin Imam Ali (as) akiwahutubia wanadamu wote amesema:


من ترک إنْصاف الضّعیف أخذه اللّه بشدید العقاب

Atakae acha kumtendea haki dhaifu, Mwenyezi Mungu atamuadhibu adhabu kali.

Utawala wa Kizayuni uliopora, ambao tangu mwanzo wa kuanzishwa kwake kwa hila, umewekwa kama chombo mikononi mwa ubeberu wa kimataifa kwa ajili ya kuleta fitna na vita katika mwili wa umma wa Kiislamu, haukuleta kwa eneo na dunia isipokuwa mauaji, uharibifu na ugaidi. Utawala huu katika historia yake yote ya uhai wa uhaini, ukiwa chini ya kivuli cha uungaji mkono wa nguvu kubwa za kimataifa, umetenda jinai nyingi dhidi ya serikali na mataifa ya eneo hili.

Hata hivyo, pamoja na yote haya, utawala wa Kizayuni, baada ya uvamizi wake wa hivi karibuni wa siku 12 dhidi ya ardhi ya Jamhuri ya Iran, ulikabiliana na kisasi kikali kutoka Iran ambacho kiliufanya udhalilike na kuchanganyikiwa, tukio hili kubwa ni bishara ya kurejea kwa umma wa Kiislamu katika zama za heshima na nguvu zake na pia ni dalili ya kukaribia mwisho wa uhai mchafu wa utawala huu.

Ndugu na dada wapendwa, wapenda haki duniani,

Watoto wa umma wa Kiislamu, hususan wanazuoni, wasomi na wakuu:

Leo hii, tukivutiwa na mwongozo wa Qur’ani Tukufu na mwenendo na sunna ya Mtume Mkuu (saw) na Ahlul-Bayt wake watakatifu, tunatangaza yafuatayo:

Kuwa na aina yoyote ya uhusiano wa kisiasa, kiuchumi au kitamaduni na utawala huu wa kupora ni kushiriki katika dhambi, uvamizi na dhuluma ambayo Mwenyezi Mungu ameikataza:

ولا تعاونوا علی الْإثْم والْعدْوان

Na wala msisaidiane katika dhulma na uadui
(Al-Maida: 2)

Kuwasaidia na kuwapa msaada watu wanyonge wa Palestina, hususan watu wa Ghaza wenye njaa na waliodhulumiwa, kwa kupeleka chakula na dawa, na kwa msaada wa kisiasa, kisheria, kikatiba, kidiplomasia na kifedha, ni jukumu la kisheria, kibinadamu na kimaadili, kwani Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: 


من أشبع جائعًا أشبعه اللّه یوم القیامة

Mwenye kumshibisha mwenye njaa, Mwenyezimungu atamshibisha siku ya Qiyama.

Lakini huenda jambo muhimu zaidi katika hatua hii nyeti ni ulazima wa kuufahamisha umma wa Kiislamu na wapenda haki wote duniani kuhusu hatari ya jinai kama vile mauaji ya kimbari na kuhama kwa lazima, na jitihada za kuitawala ardhi hii, ambazo utawala wa Kizayuni unazifanya.

Tuna imani ya hakika kwamba mipango ya uvamizi na uharibifu ya utawala huu, kwa baraka ya uelewa wa umma wa Kiislamu, hatua za serikali huru na pia juhudi za wanaharakati huru kote duniani, itashindwa na kusukumwa nyuma.

والسلام علی من اتبع الهدی

والسلام علیکم ورحمة الله وبرکاته

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha